Home Habari za michezo MCHAMBUZI:- TUSIJIDANGANYE…TAIFA STARS NI WAKAIDA MNOO MBELE YA ALGERIA….

MCHAMBUZI:- TUSIJIDANGANYE…TAIFA STARS NI WAKAIDA MNOO MBELE YA ALGERIA….

KOCHA YANGA... AITWA TAIFA STARS...AOMBWA KUONGEZA NGUVU UFUNDI

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka East Africa Radio, Samwel Rashid mwenyewe anajiita Wakanda Republic amedai kuwa wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania ni wa daraja la kati hivyo itakuwa ngumu kupambana na wachezaji wakubwa wenye uzoefu kutoka taifa la Algeria.

kauli hiyo ya Samwel imekuja ikiwa ni saa kabla ya Taifa Stars kuvaana na Algeria, leo Septemba 7, 2023 kuwania kufuzu Fainali za AFCON 2023, mchezo utakaopigwa nchini Algeria.

“Kuhusu suala la experience ndio tunaweza tukasema hawa wachezaji wamewahi kupita kwenye hayo mazingira (mazingira ya kucheza mechi kubwa zenye presha).

“Ila suala kubwa ni je, viwango walivyonavyo (wachezaji wetu) vinaweza kulingana na mechi wanayoenda kukutana nayo? Obvious unaenda kucheza na Algeria, ingekuwa Stars anaenda kucheza na Niger tungesema okay hawa wachezaji wanahitaji motivation.

“Mfano hebu angalia daraja la ubora lililopo kati ya Sure Boy na viungo wa timu ya taifa ya Algeria? Hebu angalia midfield wa Algeria wamemuacha vitu vingapi Sure Boy?, kunazia experience, quality, mazingira ambayo amekulia, exposure yaani kila kitu.

“Timu yetu ya taifa kiuhalisia ni timu ya daraja la kati sana, ni timu ambayo unaweza ukasema ni timu ya kawaida sana, hatuna wachezaji wengi wenye kariba kubwa, hatuna wachezaji wengi ambao wanauwezo wa ku-deliver vile ambavyo watu tunataka,” amesema Wakanda Republic.

SOMA NA HII  AHMED ALLY:- KWA UBORA WA SASA TULIONAO SIMBA...UBINGWA WA LIGI NI HALALI YETU...