Habari za michezo
SKUDU KAMA NZEGELI SASA, MAMBO YAPO HIVI
Staff Desk
September 8, 2023
6:56 am
Winga wa Yanga Skudu Makudubela ameamua kupita njia za kiungo wa Yanga raia wa Congo Maxi Mpia Nzengeli.
Skudu ameonekana jana katika mazoezi ya Yanga akichomekea kama Nzengeli ambae amekuwa maarufu kwa Mashabiki wa kandanda nchini kwa style yake hiyo.
Yanga wanaendelea na mazoezi wakijiandaa na mchezo wao wa kwanza wa Raundi ya mwisho ya mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya El Merreikh ya Sudan Septemba 16, mwaka huu Uwanja wa Pele Jijini Kigali nchini Rwanda.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.