Habari za SImba SC
Habari za michezo

HAKUNA SIMBA BILA CHAMA SHABIKI AFUNGUKA

Staff Desk September 13, 2023 12:14 pm

Shabiki kindakindaki wa Klabu ya Yanga ambaye pia ni mchambuzi wa soka, Jimmy Kindoki amesema kuwa Klabu ya Simba inategemea mchezaji mmoja tu ambaye ni Clatous Chota Chama raia wa Zambia, na siku akiondoka timu itakufa.

Kindoki ambaye pia anamiliki leseni ya ukocha amesema hayo kupitia kipindi cha KipengaXtra cha EA Radio wakati wakijadili mambo mbalimbali yanayohusu soka la Bongo.

“Tunaposema uimara wa timu ni kwamba kwenye kila nafasi kwanza hakuna mchezaji tu mmoja anayetegemewa maana yake kuna nafasi zaidi ya mchezaji mmoja kwenye kila nafasi.

“Lakini hao hao wachezaji wamekamilika technically, kwamba Mwalimu akija hata akibadili mfumo wakati mechi inaendelea wachezaji wanaweza ku-copy na mazingira fasta na mechi ikampa matokeo.

“Kitu kama hicho huwezi kukipata Simba, Simba akiondoka Chama tu timu imekufa hapo hapo,” amesema Jimmy Kindoki.

MBRAZILI AMALIZA KAZI YA DYNAMO……….., GAMONDI AWAFANYIA UMAFIA WAARABU YANGA YAPAA AFRIKA YASHIKA NAMBA MOJA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

One response to “HAKUNA SIMBA BILA CHAMA SHABIKI AFUNGUKA”

  1. Francisco says:

    Hakuna kitu kama hicho kusema kwamba simba inamtegemea mchezaji huko ni kuitusi timu kwamba haina uwezo wowote bila chama sisi tunajiamini na tunaweza hata asipokuwepo MIMI NI FRANCISCO SHABIKI LA SIMBA DAM DAMU UTANIAMBIA NINI WEWE

Leave a Reply