Home Habari za michezo BAADA YA KUPATA ‘PANCHA’ INGINE….KRAMO NNJE WIKI MBILI….

BAADA YA KUPATA ‘PANCHA’ INGINE….KRAMO NNJE WIKI MBILI….

Habari za Simba

Mmoja wa viongozi wa benchi la ufundi Simba amesema mchezaji Aubin Kramo ataukosa mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Power Dynamos kwasababu ya majeraha aliyoyapata ya goti.

Chanzo hicho kimeithibitisha kuwa kutokana na majeraha aliyoyapata mchezaji huyo aliyejiunga na Simba msimu huu atakaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili.

“Amepata majeraha ya goti anatarajia kupona baada ya wiki mbili, hivyo ataukosa mchezo wa kwanza lakini mchezo wa pili tutaangalia hali yake kama atakuwa sawa atacheza”

Simba itacheza mchezo wa kwanza CAFCL ikiwa ugenini katika uwanja wa Levy Mwanawasa nchini Zambia Septemba 16 na kucheza mchezo wa marudiano hapa Dar es Salaam Oktoba Mosi, mwaka huu.

Kikosi cha Simba kikiwa na mastaa 20 kinaondoka jijini Dar leo Septemba 14 kwa ndege tayari kwa mchezo huo.

SOMA NA HII  GAMONDI AMPA OKRAH DAKIKA 180 ZA KUMSHAWISHI....,LA SIVYO.....