Home Habari za michezo NAMNA MTZ NOVATUS MIROSHI ALIVYOKICHAFUA JANA LIGI YA MABINGWA ULAYA…

NAMNA MTZ NOVATUS MIROSHI ALIVYOKICHAFUA JANA LIGI YA MABINGWA ULAYA…

Habari za Michezo

Kiungo wa Kimataifa wa Tanzania, Novatus Dismas Miroshi usiku wa jana amecheza kwa dakika zote 90 timu yake, FC Shakhtar Donetsk y Ukraine ikichapwa mabao 3-1 na FC Porto ya Ureno katika mchezo wa kwanza wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Volksparkstadion Jijini Hamburg, Ujerumani.

Mabao ya FC Porto yamefungwa na washambuliaji wake Mbrazil, Wenderson Galeno mawili dakika ya nane na 15 na Muiran Mehdi Taremi dakika ya 29.

Bao pekee la FC Shakhtar Donetsk inayolazimika kuchezea mechi zake za nyumbani Ujerumani kutokana na machafuko yanayoendelea nchini kwao kufuatia uvamizi wa majeshi ya Urusi limefungwa na mshambuliaji wake Mvenezueala, Kevin Kelsy dakika ya 13.

Miroshi anakuwa Mtanzania wa tatu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya Athumani Machuppa na Mbwana Samatta na mchezaji wa tatu kwa ujumla kutoka nchi hii kucheza michuano ya Ulaya baada ya Kassim Manara kucheza iliyokuwa michuano ya Kombe la Washindi.

SOMA NA HII  WAKATI SIMBA WAKICHEKELEA RATIBA YA CAF....NABI KAWATAZAMA WAPINZANI WAKE WEE..KISHA AKAGUNA NA KUSEMA HAYA...