Azam FC
BALEKE ATOA AHADI HII LEO DHIDI YA COASTAL UNION…
Staff Desk
September 21, 2023
2:18 pm
Straika wa Simba SC, Jean Baleke amesema leo, watawashushia mvua ya magoli Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.
Simba SC anashuka dimbani leo kwenye Uwanja wa Uhuru mara baada ya kutoka kwenye majukumu ya Kimataifa alipotoka kuikabili Power Dynamos ya Zambia ugenini na kupata sare ya 2-2.
Akizungumza mara baada ya kukamilisha mazoezi ya mwisho jana kwenye uwanja wa Mo Simba Arena Bunju jijini Dar, Baleke alisema leo kipigo kinawahusu Coastal Union.
“Tutafunga magoli mengi. Mimi nitafunga magoli leo,” alisema Baleke.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.