Habari za Simba SC
Habari za michezo

IWE JUA IWE MVUA SIMBA AJA NA KAULI NGUMU DHIDI YA POWER DYNAMO

Staff Desk September 27, 2023 3:46 pm

Klabu ya Simba SC, imesema iwe mvua iwe jua, lazima iwashushie kichapo Power Dynamos katika mchezo wa Klabu Bingwa Afrika utakaopigwa Jumapili, Oktoba 1, 2023 katika Uwanja wa Azam Comlex-Chamazi jijini Dar.

Ahmed Ally ambaye ni Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumzia maandalizi yao kuelekea mchezo huo utakaoamua hatima yao ya kwenda makundi baada ya ule wa awali kumalizika kwa sare ya 2-2 huko Zambia.

“Tarehe moja ya mwezi wa kumi ni siku ya Mnyama kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Sisi hatwendi kuweka historia, tunakwenda kwenye miasha yetu ya kawaida.”

“Tunafahamu mchezo ni mgumu dhidi ya Power Dynamos, wote mliona namna walivyotusumbua lakini wanakuja nyumbani Tanzania, sehemu ambayo hakuna aliyetoka salama na hicho hicho atakutana nacho. Bora wangekubali tukamalizana nao kwao,” alisem Ahmed.

SIMBA CHAP SANA WAWAHI POWER DYNAMO BREAKING NEWS : TANZANIA KUWA MWENYEJI WA AFCON 2027

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply