Home Habari za michezo BAADA YA KUONA MAMBO MAGUMU…KRAMO AOMBA KURUDI KWAO KUJIPANGA UPYA…

BAADA YA KUONA MAMBO MAGUMU…KRAMO AOMBA KURUDI KWAO KUJIPANGA UPYA…

Habari za Simba

Uongozi wa Simba SC, upo katika mipango ya kumruhusu kiungo wao, Muivory Coast, Aubin Kramo, kurejea nyumbani kwao kwa ajili ya matibabu ya majeraha yake ya goti.

Hiyo ikiwani siku chache tangu kiungo huyo, ajitoneshe majeraha hayo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ngome FC uliochezwa Simba Mo Arena, Bunju, Dar, wikiendi iliyopita.

Katika mchezo huo, Simba SC walibuka na ushindi wa mabao 60 ambao kiungo huyo alitolewa katika dakika 42 baada ya kujitonesha jeraha hilo linalomsumbua tangu ajiunge na timu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Simba SC, kiungo huyo juzi alikutana na uongozi wa timu hiyo, na kuomba arejee kwao kwa ajili ya matibabu hayo ya goti.

Mtoa taarifa huyo amesema, uongozi unafikiria kumruhusu kiungo arejee kwao, licha ya hivi sasa kusubiria vipimo ya MRI, ili kufahamu ukubwa wa tatizo lake.

“Jeraha hilo la goti limekuwa likimsumbua mara kwa mara tangu Kramo ajiunge na timu, hivyo hivi sasa yupo katika mazungumzo na uongozi kwa ajili ya kupewa ruhusa ya kurejea nyumbani kwao kujitibia.

“Mara ya pili Kramo anakaa nje ya uwanja kutokana na jeraha hilo la goti ambalo limekuwa likimtesa, hivyo ameona ni bora akarejea kwao kwa ajili ya kwenda kujitibia.

“Anachosubiria ruhusa ya viongozi pekee ambayo itamfanya arejee haraka nyumbani kwao kwa ajili ya matibabu wakati huu akisubiria majibu ya vipimo baada ya juzi kufanyiwa ambayo yatatoka leo Jumanne (Septemba 12), amesema mtoa taarifa huyo.

Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliveira Robertinho alithibitisha kupata majeraha kwa kiungo huyo akisema: “Ni kweli Kramo alipata majeraha ya goti, hivi sasa yupo chini ya uangalizi wa madaktari akiendelea kupatiwa matibabu kuhakikisha anarejea haraka uwanjani.”

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema: “Tunasikitika kuona mchezaji wetu muhimu kaumia kwa mara nyingine, tunangojea ripoti ya madaktari halafu tutawajulisha ni kwa namna gani ataendelea kusubiria.

“Uhakika ni kwamba hakupata majeraha makubwa sana safari h, hivyo yawezekana akawa hajaumia ki hivyo au madaktari wao ndio watasema nini kitajiri baada ya kupata dhuruba hiyo’ amesema.

SOMA NA HII  KAMWE:- WAARABU TUMEWASOMA...TUMEWAPIGIA MAHESABU MAKALI...WATASHANGAA MPIRA BOLIBO