Home Habari za michezo BEKI KISIKI WA SIMBA APIGWA STOP KONGO

BEKI KISIKI WA SIMBA APIGWA STOP KONGO

AISEE!! NABI AZINYAKA SIRI ZA INONGA...AWAKABIDHI MAYELE NA MUSONDA...ISHU NZIMA HII HAPA A-Z

Beki kisiki wa Simba, Henock Inonga ameshusha presha ya vigogo na mashabiki wa timu hiyo baada ya kupona majeraha na kuungana moja kwa moja na kikosi katika mazoezi yanayoendelea, Bunju baada ya mabosi vigogo kumzuia kujiunga na timu ya taifa ya DR Congo.

Inonga aliumia mkono wiki tatu zilizopita kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Singida jeraha lililomlazimu kukaa nje ya uwanja kwa majuma mawili kabla ya Jumanne iliyopita kuanza mazoezi, huku akiwa mmoja wa wachezaji walioitwa timu ya taifa ya DR Congo kabla ya kuumia.

Mchezaji huyo aliitwa ili kucheza mechi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 dhidi ya Sudan, lakini mabosi wa Simba wame-wasiliana na Shirikisho la Soka la DR Congo kuomba beki huyo asijumuishwe kikosini ili apate muda wa kutosha kupona jeraha lake.

Simba imefanya hivyo ili Inonga atumie muda huu kujinoa na kurejea kwenye utimamu wa mwili na akili, huku kocha mkuu wa kikosi hicho, Robertinho akijenga ‘ukuta wa Yericko’ kati ya maras-ta wawili Inonga na Che Malone Fondoh.

SOMA NA HII  SIMBA, YANGA WAWEKA WAZI MALENGO YA USAJILI WAO DIRISHA KUBWA LA USAJILI