Home Habari za michezo GAMONDI APEWA MAAGIZO HAYA KUHUSU AL MAREKH YA SUDAN

GAMONDI APEWA MAAGIZO HAYA KUHUSU AL MAREKH YA SUDAN

Habari za Yanga SC

UONGOZI wa Yanga ni kama umempa maagizo mazito kocha mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamond baada ya kusema kwa kuwa msimu uliopita walifika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, basi msimu huu hakuna kinachoshindikana kufikia malengo yao.

Yanga msimu uliopita walicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Algers ambapo walipoteza kwa faida ya bao la ugenini. Msimu huu mpaka sasa wapo hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wakienda kucheza dhidi ya Al Merrikh ya Sudan kuwania kutinga makundi.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, alisema: “Kila shabiki wa Yanga na Afrika nzima wanafahamu msimu uliopita Yanga tulicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, hivyo hiyo ni meseji nzito kwa Kocha Gamondi na wachezaji wapya wa Yanga wafahamu timu haitakuwa tayari kushindwa kufika mbali.

“Mwalimu tayari anafahamu kuwa msimu uliopita Yanga tulicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Aftrika, hii meseji kubwa sana kwake na inakuwa kama agizo la Yanga msimu huu kufika mbali zaidi katika michuano hii ya kimataifa ambayo tunashiriki.

“Wachezaji wageni pia wanapata ujumbe wao juu ya jambo hili kwamba Yanga inatakiwa kufika mbali kama ambavyo ilikuwa msimu uliopita.

SOMA NA HII  KISA LUSAJO VIONGOZI WAHAHA NAMUNGO