Home Habari za michezo HAKUNA SIMBA BILA CHAMA SHABIKI AFUNGUKA

HAKUNA SIMBA BILA CHAMA SHABIKI AFUNGUKA

Habari za SImba SC

Shabiki kindakindaki wa Klabu ya Yanga ambaye pia ni mchambuzi wa soka, Jimmy Kindoki amesema kuwa Klabu ya Simba inategemea mchezaji mmoja tu ambaye ni Clatous Chota Chama raia wa Zambia, na siku akiondoka timu itakufa.

Kindoki ambaye pia anamiliki leseni ya ukocha amesema hayo kupitia kipindi cha KipengaXtra cha EA Radio wakati wakijadili mambo mbalimbali yanayohusu soka la Bongo.

“Tunaposema uimara wa timu ni kwamba kwenye kila nafasi kwanza hakuna mchezaji tu mmoja anayetegemewa maana yake kuna nafasi zaidi ya mchezaji mmoja kwenye kila nafasi.

“Lakini hao hao wachezaji wamekamilika technically, kwamba Mwalimu akija hata akibadili mfumo wakati mechi inaendelea wachezaji wanaweza ku-copy na mazingira fasta na mechi ikampa matokeo.

“Kitu kama hicho huwezi kukipata Simba, Simba akiondoka Chama tu timu imekufa hapo hapo,” amesema Jimmy Kindoki.

SOMA NA HII  MASTAA HAWA WA YANGA WANAFAA PALE SIMBA KABISA

1 COMMENT

  1. Hakuna kitu kama hicho kusema kwamba simba inamtegemea mchezaji huko ni kuitusi timu kwamba haina uwezo wowote bila chama sisi tunajiamini na tunaweza hata asipokuwepo MIMI NI FRANCISCO SHABIKI LA SIMBA DAM DAMU UTANIAMBIA NINI WEWE