Home Uncategorized MISRI YAANZA AFCON NA USHINDI MWEMBAMBA DHIDI YA ZIMBABWE

MISRI YAANZA AFCON NA USHINDI MWEMBAMBA DHIDI YA ZIMBABWE



TREZEGUET AKIWA NA SALAH
Wenyeji wa michuano ya Afcon, Misri wameanza michuano hiyo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zimbabwe.

Mechi hiyo ya ufunguzi wa michuano ya Afcon kwenye Uwanja wa Taifa jijini Cairo, Misri walikwenda mapumziko wakiwa na bao 1-0, mfungaji akiwa Mohamed Trezeguet.

Hata hivyo, Khama Billiat wa Zimbabwe ndiye alikuwa msumbufu zaidi upande wa ngome ya Misri na wenyeji walilazimika kufanya kazi ya ziada kupata bao.

Zimbabwe walionekana kucheza kwa kujiamini lakini tatizo likawa ni mashambulizi dhaifu.
SOMA NA HII  CHELSEA KUPITISHA PANGA LA KIBABE