Home Habari za michezo HUKO YANGA UNAAMBIWA LEO NDIO LEO LIGI YA MABIGWA BAADA YA ...

HUKO YANGA UNAAMBIWA LEO NDIO LEO LIGI YA MABIGWA BAADA YA MIAKA 25

Yanga vs Namungo

HAKUNA Kitu kikubwa kinachozungumzwa kwenye kambi ya Yanga zaidi ya kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya miaka 25, timu hiyo inahitaji kufikia hatua hiyo siku ya leo.

Yanga leo wanashuka dimbani kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo ikiwakaribisha Al Merrikh ya Sudan mchezo wa pili, uwanja wa Azam, Chamazi Dar-es-Salaam baada ya mchezo wa kwanza kushinda bao 2-0 waliyoyapata nchini Rwanda.

Katika mchezo huo Yanga wanahitaji kushinda kwa ajili ya kucheza makundi, Al Merrikh wameahidi kupindua meza mbele mbele ya Wananchi hao ili kusonga mbele katika hatua hiyo.

Katika michezo sita ambayo Yanga imecheza msimu huu  mashindano yote, imeruhusu bao moja tu katika mchezo wa kwanza wa hatua ya kwanza ya mtoano ya CAFCL dhidi ya Asas FC ya Djibout, ilishinda jumla ya mabao 7-1.

Yanga ikishunda mabao 5-0 mbele ya KMC na kipigo cha idadi hiyo ilikutana nacho  JKT Tanzania na kuitandika bao 1-0 Namungo FC kabla ya mchezo huo , walipata ushindi wa mabao 2-0 mchezo wakwanza ya hatua ya pili dhidi ya Al Merrikh ambao walicheza nchi Rwanda.

Kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Miguel Angel Gamond ambaye anahitaji kuona wachezaji wake kuwa makini ikiwemo safu ya ulinzi ambayo ipo kwenye mikono salama na mabeki wao Bakari Mwamnyeto , Ibrahim Bacca, Attohoula Yao,  Nickson Kibabage, Gift Freddy.

Kwenye safu ya ushambuliaji Yanga imekuwa ikiongozwa na Clement Mzize, Kennedy Musonda mbali na hao pia viungo na mawinga akiwemo, Max Nzengeli,  Mudathiri Yahya na Stephen Aziz Ki wamekuwa na mchango mkubwa katika ufungaji wa timu hiyo.

Kuelekea mchezo huo Kocha wa Yanga, Gamond alisema maandalizi yameenda vizuri wachezaji  wako tayari kumalizia dakika 90 za mwisho kusaka ushindi na kufanikiwa kutinga makundi.

Alisema ameandaa vijana wake kimwili na kiakili kwa ajili ya kutafuta ushindi na kusahau matokeo ya mechi ya kwanza kama walishinda bao 2-0 na kuwataka wachezaji kuanza upya.

“Tumefanya maandalizi mazuri wachezaji wote wako tayari, haitakuwa mechi rahisi kwa sababu Al Merrikh watakuja kivingine, tunatakiwa kuwa makini kutafuta ushindi ambao tutafanikiwa kusonga mbele na kucheza makundi.

SOMA NA HII  KUELEKEA KOMBE LA DUNIA STARS YAINYOOSHEA KIDOLE MOROCCO