Home Habari za michezo KWA DATA HIZI , YANGA YA KIMATAIFA KAZI IPO

KWA DATA HIZI , YANGA YA KIMATAIFA KAZI IPO

Habari za Yanga

Ukichoma mbele ya nyota wa Yanga utakuwa umeua bendi kwa kuwa hawana kazi ndogo wao balaa lao ni kwenye kucheka na nyavu iwe kimataifa ama kitaifa.

Chini ya Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi kwenye mechi saba ambazo wamecheza kasi yao sio ya kitoto kwenye msako wa ushindi.

Hapa kwenye mwendo wa data tupo na mechi zao Yanga walizocheza namna hii:- Washambuliaji wametumwa kazi.

Safu ya ushambuliaji ya Yanga inayoongozwa na Kennedy Musonda imetupia mabao 21 kwenye mechi 7 za ushindani.

Ni wastani wa kuwa na hatari ya kucheka na nyavu kila baada ya dakika 30 wakiwa kwenye msako wa ushindi uwanjani.

Ukuta mgumu Ndani ya dakika 630 ukuta wa Yanga wenye Bakari Mwamnyeto ambaye ni nahodha, Dickson Job, Kibwana Shomari umeshuhudia bao moja likizama nyavuni kwenye mechi za ushindani.

Ilikuwa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASAS FC uliochezwa Uwanja wa Azam Complex na ilikuwa ni mwendo wa penalti walipotunguliwa. Ni kiungo mkabaji Zawadi Mauya kwenye harakati za kuokoa hatari alisababisha penalti hiyo.

Ushindi Ni mechi sita Yanga imeshinda ilizoshuka uwanjani chini ya Gamondi na ikionja joto ya kupoteza kwenye mchezo mmoja wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani zao wajadi Simba.

Ndani ya dakika 90 walitoshana nguvu kwenye mchezo huo wa fainali ubao wa Uwanja wa Mkwakwani, uliposoma Yanga 0-0 Simba katika mikwaju ya penalti ubao ukasomoa Yanga 1-3 Simba.

Mwendo wa tanotano Yanga katika mechi 7 ni mechi tatu ilishuhudia ikishinda mabao matanomatano baada ya dakika 90. Mechi moja ilikuwa ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASAS FC, mechi mbili za ligi dhidi ya KMC na JKT Tanzania.

Mitambo ya mapigo huru Katika kikosi cha Yanga wapo wataalamu wa mapigo huru wakiongozwa na Aziz KI ambaye katika mabao aliyonayo kibindoni mawili kwenye ligi moja aliwatungua JKT Tanzania dakika ya 45 akiwa nje ya 15 kwa pigo la faulo.

Mechi zake Mechi za Gamondi akiwa kwenye benchi la ufundi ndani ya kikosi cha Yanga ubao ulikuwa namna hii:- Yanga 2-0 Azam FC, Ngao ya Jamii, Uwanja wa Mkwakwani, Agosti 9, Yanga 0-0 Simba, (1-3 penalti), Ngao ya Jamii, Uwanja wa Mkwakwani, Agosti 13.

ASAS 0-2 Yanga, Ligi ya Mabingwa Afrika, Uwanja wa Azam Complex ilikuwa Agosti 20. Yanga 5-0 KMC, Ligi Kuu Bara, Uwanja wa Azam Complex Agosti 23, Yanga 5-1 ASAS FC Ligi ya Mabingwa Afrika, Uwanja wa Azam Complex, Agosti 26.

Yanga 5-0 JKT Tanzania, mchezo wa ligi Uwanja wa Azam Complex, Agosti 29, Al Merreikh 0-2 Yanga, mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Uwanja wa Pele Kigali.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI