Home Uncategorized AZAM TV WAIBUKA KIVINGINE NA APP YA KISASA ZAIDI YA MAX

AZAM TV WAIBUKA KIVINGINE NA APP YA KISASA ZAIDI YA MAX


Uongozi wa Azam Media jana Ijumaa umefanya uzinduzi wa application ‘App’ mpya inayojulikana kama Azam Tv Max, ambayo inatakuwa maalumu kwa ajili ya wateja wa Azam TV itakayokuwa ikipatikana kupitia simu ya mkononi.

Application hiyo ni mbadala wa ile ya awali ambayo kwa sasa imeboreshwa zaidi na inawapa watumiaji fursa ya kutazama chaneli nyingi na vipindi mbalimbali vya televisheni vikiwemo vipindi mubashara na vile vilivyorekodiwa.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Tido Mhando amesema kuwa, mtumiaji wa kisimbuzi cha Azam TV ambaye amelipia kadi yake atafaidi uhondo wote wa Azam Tv Max bila malipo yoyote ikiwemo kuangalia mechi za Ligi Kuu ya Tanzania inayoendelea kwa sasa.

“Tumeamua kuwarahisishia watu wetu ambao hawatakuwa karibu na TV, hivyo kupitia Azam Max wataweza kufaidi vipindi vyetu vyote ambavyo vinapatikana kwenye ving’amuzi vyetu ikiwemo kuangalia mpira wa ligi yetu mubashara (Live).

“Hivyo wateja ambao walishajisajili awali watatakiwa kujisajili upya ili kuweza kupata huduma ya Azam Tv Max kwenye simu zao wajipatie uhondo wa video mbalimbali, kama vile tamthilia na vipindi vya watoto,” alisema Mhando.
SOMA NA HII  MAKAMBO RUKSA KUTUA YANGA,NDANI YA CHAMPIONI JUMATANO