Home Habari za michezo ROBERTINHO AFUNGUKA HAYA KUHUSU LUIS MIQUISSONE

ROBERTINHO AFUNGUKA HAYA KUHUSU LUIS MIQUISSONE

Habari za Simba SC

Kocha Robertinho amesema amefurahishwa na kitendo cha winga Luis Miquissone kupungua uzito, akisema kurejea kwake kwenye kiwango na wepesi kutaiongezea kitu kizito timu yake huku pia akisubiri taarifa njema za kipa aliyekuwa majeruhi, Aishi Manula.

Kocha alisema Luis alirejeshwa Simba akiwa na uzito wa kilo 77, lakini hadi sasa jamaa amekata kilo nne na kubaki na 73 ambazo zimemrudisha kwenye wepesi na juzi akifunga bao lake kwenye mechi ya kirafiki ya kujipima nguvu dhidi ya Kipanga.

“Jambo zuri kuna wachezaji wetu wengine wameanza kuimarika angalia Miquissone (Luis) ni mchezaji mkubwa ambaye anajua kuamua mechi kubwa kama hizi sasa amepungua uzito anarudi kwa kasi kwenye kiwango chake, Inonga (Henock) amerejea pia tunasubiri kusikia taarifa njema kuhusu Manula (Aishi).”

SOMA NA HII  MWANZILISHI WA SIMBA DAY ATIA HURUMA..ANAISHI KWA MATESO...AMTAJA MO DEWJI..SIMBA WATOA TAMKO...