Home Habari za michezo YANGA NJIA NYEUPE, HII NDIO HALI YA AL MARREIKH

YANGA NJIA NYEUPE, HII NDIO HALI YA AL MARREIKH

Habari za Yanga

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka East Africa Radio, Master Tindwa amesema kuwa wapinzani wa Yanga SC kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, AL-Merreikh walikutana na timu ngumu kutoka Congo DR tofauti na Yanga ambao walikutana na ASAS FC ya Djibout.

Tindwa amesema hayo kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Merreikh ya Sudan utakaopigwa Septemba 16, 2023 nchini Rwanda.

“Ubora wa timu aliyokutana nayo Al-Merreikh na timu aliyokutana nayo Yanga ni tofauti, Wacongo ni wagumu, Yanga alikutana na Asas wepesi ambao waliwafunga saba, ushindi wa goli saba kwenye mashindano haya ni mkubwa sana, kwa hiyo tunahitaji tuone wakikutana itakuwaje,“ amesema Master Tindwa.

Kwa uoande wake, mchambuzi Samwel Rashid mwenyewe anajiita Wakanda Republic amesema kuwa ubora wa Kikosi cha Merreikh msimu huu sio mzuri ikilinganishwa na Ubora wa Yanga kwani wachezaji wengi wazuri wa timu hiyo wameondoka kutokana kutokana na hali ya amani kuwa mbaya nchini humo.

“Quality ya wachezaji waliopo ndani ya kikosi cha Al-Merrikh kidogo imepungua, kwa sababu wale wachezaji wake wengi nyota waliweza kuvunja mikataba na hiyo timu kutokana na machafuko yanayoendelea nchini Sudan.

“Sio tu wachezaji, bali benchi la ufundi pia, pamoja hata na rais wa timu ya Al-Merrikh aliweza kuondoka nchini Sudan akaenda kuishi uhamishoni nchini Morocco,” amesema Wakanda.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JJUMATANO