Habari za Simba SC
Habari za michezo

BAADA YA KUPIGA MPIRA PAPATUPAPATU SIMBA WAOMBA UTULIVU SASA

Staff Desk October 5, 2023 2:03 pm

Kutokana na kikosi cha Simba kucheza mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika mpira papatupapatu, Kocha Mkuu wa Simba Robert Oliveira ameweka wazi kuwa watafanya vizuri.

Kwenye mchezo wa ugenini dhidi ya Power Dynamos ubao ulisoma Power Dynamos 2-2 Simba na mabao ya Simba ni Clatous Chama alifunga.

Ule wa pili ubao ulisoma Simba 1-1 Power Dynamos ambapo ni Kondwani Chidon alijifunga.

Leo, Simba ina kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

“Sikiliza, mpango ni kupata matokeo na kucheza soka la kuvutiana tunaweza kufanya hivyo kutokana na wachezaji tulionao kwenye kikosi,”.

Ni mechi moja imecheza Simba ugenini ilikuwa dhidi ya Mtibwa Sugar ubao ulisoma Mtibwa Sugar 2-4 Simba.

YANGA YATOA TAMKO HILI BAADA YA KUSHINDWA KUTAMBA MBELE YA IHEFU JE SIMBA WATAENDELEZA UBABE LEO!?

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply