Home Habari za michezo HUU HAPA UKWELI KUHUSU AL AHLY KUJA NA MAPIPA BONGO….KUMBE MCHONGO NI...

HUU HAPA UKWELI KUHUSU AL AHLY KUJA NA MAPIPA BONGO….KUMBE MCHONGO NI TOKA ….

Habari za Michezo leo

Guys hawa ni Al ahly timu bora Africa na dunia kote,hawa ni mabingwa mara (43) wa Ligi ya kwao pia wana CAF Champions (11) bila kusahau Super Cup (8) n.k

Hawa jamaa wanajua kucheza mechi za mtoano kwani wanaamini wao walizaliwa kushinda Vikombe.

Mimi Binafsi sijashangaa kuwaona na Mapipa+chakula kwani hii siyo mara yao ya kwanza kubeba nyenzo muhimu kwenye mechi muhimu.

Kumbukumbu zinaonyesha walibeba nyenzo zao muhimu dhidi ya Al hilal omdurman,pia walifanya hivyo kwenye mechi ya fainali dhidi ya Wydad Casablanca.

Kwa kifupi wanalijua vizuri soka la Africa na vibweka vyake,na tukumbuke hawa jamaa wamefungwa mara mbili ndani ya miaka mitano waliyokuja Tanzania hivyo wanajua wapi walijikwaa.

Al ahly wanajua fika haya mashindano yana utajiri mkubwa hivyo hakuna chumba cha wao kufanya makosa.

Wanajua kabisa Dar es Salaam kuna joto tofauti na kwao hivyo wamebeba mapipa ya kumimina barafu ili wachezaji wao wapate Recovery nzuri.

Al ahly wanajua mpinzani wao anacheza mpira wa nguvu hivyo wameamua kubeba chakula chao cha asili ili wachezaji wao wapate nguvu ya kupambana.

Watanzania hili tulichukue kama Somo next time timu zetu zikisafiri kwenda nje ni vyema zikabeba vyenzo muhimu ili kuepuka matatizo ya hapa na pale….hata Guinea walifanya hivyo kwenye Afcon ya 2019 Misri.

SOMA NA HII  PAMOJA NA YANGA KUONGOZA LIGI...GSM AGUNA KISHA AFANYA KUFRU BAB KUBWA HUKO...MWAKALEBELA ATIA NDIMU...