Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita tangu tuanze safari ya Mabadililko Klabu yetu imepiga hatua kubwa sana katika nyanja mbali mbali.
Pamoja na maendeleo ambayo Klabu yetu imepiga katika kipindi hiki cha miaka mitano lakini malengo yetu bado hatujayafikia.
Mojawapo ya majukumu yangu kama Raisi wa heshima wa Simba ni kuhakikisha Uongozi na Utawala bora unazidi kuboreshwa kila wakati ili kuzidi kusukuma gurudumu la maendeleo ya Klabu yetu.
Hivyo basi baada ya kushauriana na Mwenyekiti wa Bodi na Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, nimewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Baraza la Ushauri ( Advisory Board) la Klabu ya Simba.