Home Habari za michezo MASTAA HAWA UANGA WAITAMANI SIMBA KUFA KUPONA DABI YA KARIAKOO

MASTAA HAWA UANGA WAITAMANI SIMBA KUFA KUPONA DABI YA KARIAKOO

Geita vs Yanga

Wakati kiungo mshambuliaji wa Yanga kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Maxi Nzengeli akisema anajisikia furaha kuona mabao aliyofunga katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida Fountain Gate yameipatia timu yake pointi tatu muhimu, ameweka wazi nguvu zao sasa zimehamia kujipanga kuifunga Simba.

Nzengeli alifunga magoli mawili katika ushindi wa mabao 2-0 wakati mabingwa hao watetezi walipoikaribisha Singida Fountain Gate katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam juzi.

Ushindi huo uliifanya Yanga ifikishe pointi 18 na kuendelea kukaa kileleni katika msimamo wa ligi hiyo yenye kushirikisha timu 16.

Akizungumza na gazeti hili, Nzengeli alisema alitamani kufunga hat-trick katika mechi hiyo lakini anasikitika hakupata nafasi hiyo.

Nyota huyo alisema anaimani kubwa ya kuendelea kufanya vizuri katika kila mechi na timu yao kufikia malengo wanayotarajia ikiwamo kutetea taji la ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

“Tumepata matokeo mazuri, bado tuna michezo mingine mbele yetu, tutahakikisha tunashinda. Ikiwamo mechi ya Simba ambao ni wapinzani wetu katika mbio za ubingwa.

Hizi pointi tatu zimetusaidia na kutuweka katika nafasi nzuri, Singida Fountain Gate wameingia katika mfumo wetu, tunamaliza mechi hii tunaenda kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Simba,” alisema Nzengeli.

Aliongeza anaamini wachezaji wote wa Yanga wataendelea kujituma katika kila mechi wanayocheza kwa sababu wanahitaji kumaliza msimu kwa mafanikio makubwa.

“Kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kuendelea kusapoti timu yao, tunaimani ya kufanya vizuri kwa sababu tunahitaji kutetea taji la ubingwa, lazima tupambane tushinde mechi yetu ijayo,” aliongeza Mkongomani huyo.

Katika mechi hiyo, Nzengeli alifunga bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 30 na la pili dakika nane baadaye.

Simba na Yanga zitakutana katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu itakayochezwa Novemba 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

SOMA NA HII  ISHU YA BALE YAMKASIRISHA RAIS