Home Habari za michezo BAADA YA ‘KUUBONDA’ VYA KUTOSHA JANA..HATMA YA AZIZ KI , PACOME KUJULIKANA...

BAADA YA ‘KUUBONDA’ VYA KUTOSHA JANA..HATMA YA AZIZ KI , PACOME KUJULIKANA LEO YANGA..

Habari za Yanga

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Stephane Aziz Ki, leo anatarajiwa kufanyiwa vipimo zaidi ili kufahamu ukubwa wa jeraha lake.

Aziz Ki aliumia sehemu ya chini ya mguu katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Fountain Gate uliochezwa jana Ijumaa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kiungo huyo katika mchezo huo, alitolewa uwanjani kipindi cha pili na nafasi yake ikachukuliwa na Clement Mzize.

β€œAziz Ki aliumia sehemu ya chini ya mguu, tunakwenda kumfanyia vipimo leo kupata taarifa kamili ya ukubwa wa jeraha lake,” alisema Daktari wa Yanga, Moses Etutu.

Katika hatua nyingine, Kiungo wa Yanga, Pacome Zouzoua, baada ya kupata maumivu katika mchezo wa jana dhidi ya Singida Fountain Gate, kwa sasa yuko sawa.

Pacome alipata maumivu ya goti baada ya kugongana na mchezaji wa Singida katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC ambao Yanga waliibuka na ushindi wa magoli 2-0.

Daktari wa Yanga, Moses Etutu, amesema: β€œPacome aligongana na mchezaji wa Singida na kupata maumivu ya goti, lakini baada ya kupata dawa za kutuliza maumivu amekuwa sawa.”

Pacome katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, hakumaliza dakika tisini, alitoka kipindi cha pili na kuingia Skudu Makudubela.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA WAMOROCCO..CHAMA AMWAGIA SIMBA SIRI ZA BERKANE..ATOA ONYO HILI...