Home Habari za michezo GAMONDI AIPIGA CHABO SIMBA KWA MKAPA….

GAMONDI AIPIGA CHABO SIMBA KWA MKAPA….

Habari za Michezo

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi na Meneja wa timu hiyo Walter Haryson wametinga katika Uwanja wa Mkapa kutazama mchezo wa Ligi kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Ihefu.

Gamondi ameingia mapema kwenye uwanja nusu saa kabla ya mchezo huo kuanza na kushuhudia wachezaji wa timu hizo wakipasha misuli joto.

Gamondi amefika uwanjani kwa ajili ya kuwatazama wapinzani wao Simba ambao watakutana mchezo unaofuata Novemba 5 mwaka huu katika uwanja huo huo.

Kocha huyo amekuwa na utaratibu wa kwenda kutazama mechi wapinzani wao Simba kwani hata kwenye mchezo wa African Football League dhidi ya Al Ahly alikuwepo uwanjani.

SOMA NA HII  KUPITIA EXPANSE STUDIO...MERIDIANBET WANAKUJIA NA SLOT YA KIJANJA YA ROULETTE...