Home Habari za michezo HAKUNA SILLAH WALA ONANA MWAMBA HUYU HAPA

HAKUNA SILLAH WALA ONANA MWAMBA HUYU HAPA

habari za simba

Unaweza ukawa unajiuliza huyu Max Mpia Nzengeli hiki ambacho anakifanya Yanga ni kama vile mara yake ya kwanza ila hapana; huyu mwamba huu ni mwendelezo wake.

Maana msimu uliopita kabla ya Ligi Kuu ya nchini DR Congo (Linafoot) haijasimama Mbappe wa Bongo Max Nzengeli katika mechi 8 alifunga magoli 4 na kutoa Assist tatu ambapo jumla alihusika katika magoli 7.

Msimu huu wa kwanza akiwa na Mabingwa watetezi Yanga anafanya mwendelezo wa kile ambacho ametoka nacho kule DR Congo,Hadi sasa Max Mpia Nzengeli amehusika katika mabao matano kwenye mechi 5. Jamaa amefunga goli 3 na Assist 2,What a Player!!

Hiki anachokifanya Mbapee wa Bongo sifa kubwa ziende kwa Rais wa Yanga Eng Hersi Said na watendaji wake ambao walifanya saka nyoka na kwenda kusajili hiki kipaji kutoka DR Congo. Hadi sasa Max Nzengeli ndio usajili bora nchini hakuna Willy Onana wala Gibril Sillah.

SOMA NA HII  AHMED ALLY ASEMA HAYA KUHUSU WYDAD SIO POA