Home Habari za michezo KUELEKEA DAR DERBY….YANGA WAANZA KUILIA ‘TIME’ AZAM FC….

KUELEKEA DAR DERBY….YANGA WAANZA KUILIA ‘TIME’ AZAM FC….

Habari za Yanga

Benchi la Ufundi la Young Africans, limeanza kukiandaa kikosi chao kuhakikisha kinakuwa bora kabla va kukutana na Azam FC, katika mchezo wa Mzunguuko wa sita wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Young Africans itakuwa mwenyeji wa mchezo huo ambao utachezwa Oktoba 25, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Angel Gamondi, amesema anaamini uwezo wa nyota wake pamoja na mazoezi waliyoanza kufanya utawapa pointi tatu muhimu katika mchezo huo.

Gamondi amesema ameanza mazoezi ya nguvu na nyota wake kuhakikisha wanakuwa imara kila upande, anatambua Azam FC kuwa wapo bora lakini hawatokubali kupoteza mchezo huo.

“Kila mchezaji anatambua wajibu wake, tupo vizuri kila nafasi na tunaendelea kuwa imara katika sehemu chache ambazo zilikuwa na kasoro, kikubwa tunataka ushindi wa mabao mengi mbele ya Azam FC” amesema.

Kocha huyo amesema anaamini hata Azam FC wanafanya maandalizi lakini kutokana na kuhitaji kutetea taji hawatoruhusu kupoteza mchezo wa pili ligi ikiwa bado mbichi.

“Ligi ikiwa mbichi ndio wakati wa kupata matokeo mazuri, kwa sabaabu mwishoni ndio kunakuwa kugumu hivyo tunatakiwa kupambana haswa kuhakikisha tunapata matokeo mazuri,” amesema.

Meneja wa ldara ya Habari na Mawasiliano ya Azam FC, Thabit Zacharia, amesema wameanza maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Young Africans, wanaamini watafanya vizuri kutokana ubora walionao.

“Tumeanza maandalizi na tupo vizuri, kila mmoja anatambua nini anatakiwa kufanya katika mchezo huo, tunaendelea na maandalizi tukisubiri muda tu,’ amesema

Katika Ligi Kuu Tanzania Bara, timu hizo zimekutana mara 30, Young Africans imeshinda michezo 12, zimetoka sare mara tisa wakati Azam FC ikishinda michezo tisa.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUANZA KUTUPIA SIMBA SC...NTIBAZONKIZA AWACHANA WANAYANGA...