Home Habari za michezo KWA HILI LA YANGA, SIMBA INAPATA TABU SANA

KWA HILI LA YANGA, SIMBA INAPATA TABU SANA

Kinachowateza zaidi Simba ni Yanga, hizi timu ili wewe u-enjoy ni wakati unafanya vizuri mwenzio awe anafanya vibaya.

Kama timu zote zinafanya vizuri basi itatafutwa inayofanya vizuri zaidi ili meadi tu kuwe na tofauti.

Nasema Yanga ndio inawatesa zaidi Simba kwa sababu Simba ina historia ya kufanya vizuri na kuiacha mbali Yanga.

Yanga ikapambana hadi imefikia ubora wa Simba na sasa timu zote zipo kwenye daraja moja la kiuchezaji na kiushindani.

Kwa sababu Simba hawajapiga hatua nyingine mbele, presha ya Yanga imeshawachukua na sasa hivi Simba inaonekana kama imeshuka uwezo kwa sababu miaka kadhaa nyuma Yanga haikuwa hapa ilipo leo.

SOMA NA HII  MANARA ARUKA NA SIMBA KISA INONGA