Home Habari za michezo MASTAA HAWA YANGA WAITWA TIMU ZA TAIFA

MASTAA HAWA YANGA WAITWA TIMU ZA TAIFA

Habari za Yanga SC

Wachezaji watatu wa kigeni Yanga SC, kipa wa Kimataifa wa Mali, Djigui Diarra na viungo Mganda Khalid Aucho na Mburkinabe Stephane Aziz Ki wamekwenda kujiunga na timu zao za taifa.

Kikosi cha Yanga kinaendelea na mazoezi baada ya kurejea Dar es Salaam kutoka Mwanza ambako Jumamosi waliichapa Geita Gold 3-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya NBC Uwanja wa CCM Kirumba.

Haijajulikana Kocha Mualgeria wa Taifa Stars, Adel Amrouche ataita wachezaji wangapi wa Yanga kwenye kikosi chake, maana sera zake kwa sasa kutotangaza kikosi katika vyombo vya Habari.

SOMA NA HII  MCONGO ALIYEMALIZANA NA YANGA DAU LAKE LAVUNJA REKODI YA LUIS