Home Habari za michezo ROBERTINHO: NIACHIENI MIMI TUTAWASHANGAZA WA MISRI NYUMBANI KWAO

ROBERTINHO: NIACHIENI MIMI TUTAWASHANGAZA WA MISRI NYUMBANI KWAO

Habari za Simba

“Niachieni mimi,” hiyo ni kauli ya Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ baada ya kuulizwa maandalizi yake kuhusu mechi ya marudiano ya African Football League dhidi ya Al Ahly itakayopigwa kesho Jumanne, baada ya ile ya ufunguzi iliyopigwa Dar es Salaam kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Simba ipo jijini Cairo na leo itafanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na mechi hiyo ambayo inahitaji ushindi au sare ya mabao matatu ili kusonga mbele katika nusu fainali ya michuano hiyo mipya.

Akizungumza na Mwanaspoti, Robertinho alisema anatambua ugumu wa mechi hiyo, lakini suala la kupata matokeo chanya ugenini aachiwe yeye na wachezaji wake kwani wameandaa mkakati ambayo inaweza ku-washangaza wengi.

Robertinho alisema mechi ya Dar es Salaam ilimpa picha sahihi ya namna ya kucheza ugenini na kikosi chake kipo tayari kuishangaza Afrika na dunia kwa ujumla.

“Najua ugumu wa Al Ahly ikiwa nyumbani, pia najua kiu yao ya kusonga mbele ipo kwa kiasi gani. Hilo ni-achieni mimi na wachezaji tunajua tunachokifanya,” alisema Robertinho na kuongeza;

“Tupo hapa kupambana, tunataka matokeo yatakayotufanya kusonga mbele, tunaamini tutafanya vizuri zaidi.”

Mfungaji wa bao la kwanza la Simba kwenye mechi ya mkondo wa kwanza iliyopigwa kwa Mkapa Ijumaa ili-yopita, Kibu Denis alisema anaamini chama lake litapenya mbele ya Al Ahly.

“Ahly ni timu kubwa lakini hata sisi ni wakubwa, kila kitu kinawezekana kwenye soka. Tuna timu nzuri na kila mchezaji anajituma huku tukiwa na ushirikiano wa kutosha,” alisema Kibu na kuongeza;

“Zitakuwa ni dakika 90 za nguvu, tutapambana hadi mwisho na lengo ni kutinga nusu fainali.”

Simba tayari imekunja zaidi Dolla 1000 000 zaidi ya Tsh 2.4 bilioni kwa kushiriki michuano hiyo na kama itaiondosha Al Ahly na kwenda hatua inayofuata ya nusu fainali itapata mkwanja mwingine, Dolla 1700000 zaidi ya Tsh 4.2 bilioni za Kitanzania.

Ili kuhakikisha mkwanja huo unaingia kwenye akaunti za benki za Wanamsimbazi hao, uongozi wa juu wa Simba umewawekea bonasi ya bilioni moja wachezaji na benchi la ufundi ikiwa ni motisha ya kuiondosha Al Alhy.

SOMA NA HII  JINSI PACOME ALIVYOINUSURU YANGA KWENYE HATARI YA WARABU