Home Habari za michezo SIRI YA KIBU KUTAMBA SIMBA YAFICHUKA…….STORI KAMILI IKO HIVI

SIRI YA KIBU KUTAMBA SIMBA YAFICHUKA…….STORI KAMILI IKO HIVI

Habari za Simba

Mshambuliaji wa Simba SC, Kibu Denis ni miongoni mwa nyota tegemeo kwa sasa ndani ya kikosi cha Msimbazi. Panga pangua, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ lazima akipanga kikosi chake lazima yumo.

Wachambuzi mbalimbali wanapomzungumzia Kibu, wanasema kinachomfanya apate nafasi ya kuwa chaguo la kwanza kwenye kikosi ni upambanaji wake. Anajua kukaba, ana nguvu, kasi na mara kadhaa anafunga.

Hili la kufunga linaweza lisitokee mara kwa mara lakini, mchango wake huo mwingine ndio unaompa ‘kiburi’ Robertinho kumtumia hususan kwenye mechi zile ngumu.

Takwimu zake kwenye Ligi Kuu msimu huu, katika mechi ya raudi ya saba, Kibu ana assist mbili na hana goli hata moja. Mwalimu anamtumia zaidi kushambulia akitokea pembeni lakini pia mara kadhaa mwalimu amempanga kushambulia kutokea katikati.

Kibu ni miongoni mwa nyota ambao wanaa asilimia kubwa ya kuanza kwenye kikosi cha Robertinho kitakachoanza dhidi ya Yanga Novemba 2, 2023 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

SOMA NA HII  WALIOMSHAMBULIA SHABIKI WA YANGA KUADHIBIWA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here