Home Azam FC HUKO AZAM SIO POA UNAAMBIWA MASTAA HAWAMTAKI KOCHA…….HUKU MABOSI NAO WAZIBA MASIKIO

HUKO AZAM SIO POA UNAAMBIWA MASTAA HAWAMTAKI KOCHA…….HUKU MABOSI NAO WAZIBA MASIKIO

Kocha Mpya Azam FC

Hatimaye jinamizi la makocha kukataliwa na wachezaji wa Azam FC limeibuka tena kama ambavyo hutokea kila mwaka.

Katika umri wake wa miaka 15 kwenye Ligi Kuu, Azam FC imewahi mara moja tu kuanza msimu na kumaliza na kocha mmoja.Msimu huo ni 2011/12 pale Mu ingereza John Stewart Hall alipotoboa.

Baada ya hapo hakuna kocha mwingine aliyeweza, hata yeye mwenye alishindwa licha ya kuondoka na kurudi mara mbili baadaye.

Na mara zote hizo, tatizo huwa wachezaji kuwakataa makocha.

Yousouph Dabo ni kocha wa 17 kwa Azam FC. Na hapo bila kuwataja makocha waliokalia benchi la ufundi kwa kipindi cha mpito. Neider Dos Santos – Brazil,

Itamar Amorin – Brazil,

Stewart Hall – England,

Boris Bunjak – Serbia,

Stewart Hall – England,

Joseph Omog – Cameroon,

Stewart Hall – England,

Zeben Fernandes – Hispania,

Aristica Cioaba – Romania,

Hans van der Pluijm – Uholanzi, Etienne Ndayiragije – Burundi,

Aristica Cioaba – Romania

na George Lwandamina – Zambia.

Wengine ni Abdihamid Moallin – USA, Dennis Lavagne – France, Kali Ongala – England na Yousouph Dabo – Senegal

Makocha hawa wote waliondoka kwa namna moja nyingine kwa kukataliwa na wachezaji. Habari za uhakika ni kwamba safari hii ni zamu Yousouph Dabo.

Kocha huyo mwenye leseni A ya UEFA aliyoipata Ufaransa, alijiandaa kukabiliana na tatizo la kukataliwa na wachezaji ambalo tayari alikuwa analijua kuwa ni tatizo sugu la wachezaji wa Azam FC. Baada ya kuishi nao kwa siku zote hizo, hatimaye sasa jipu limepasuka. Habari za ndani kwamba Mkasa wa Dabo ulianza siku ya mazoezi ya kwanza baada ya mchezo dhidi ya Yanga. Baada ya kichapo, Dabo aliwakosoa wachezaji wake mazoezini akiwalaumu kwa kucheza chini ya kiwango na kutofuata maelekezo yake.

Akaenda mbali na kuwaambia kwamba wachezaji wasijione wako salama, dirisha dogo linakuja na atamuondoa mchezaji yoyote ambaye hawezi kufanya kama anavyotaka yeye.

Kauli hii iliwakera wachezaji na kuanzia hapo wakakubaliana kwamba wafanye wanavyoweza kufanya ili afukuzwe.

Kabla ya mchezo wowote wachezaji huwa na zoezi la kupasha moto misuli. Kwenye mchezo dhidi ya Namungo, baada ya zoezi la kupasha moto misuli, Dabo akawaambia wachezaji wake kwamba watapoteza mchezo huo kwa sababu hawakuonesha kama wako tayari kwa mchezo. Moto ukaendelea kuwaka.

Na kama ambavyo kila mtu aliona, ndivyo hali ilivyokuwa. Azam FC ikapoteza kwa mabao 3-1 huku Azam FC ikicheza kwa ari ya chini sana.

Na kwa taarifa za ndani ni kwamba wachezaji wamepanga kumhujumu Dabo kwenye michezo ijayo hadi afukuzwe. Wanalalamika kwamba ni kocha mkali sana na hataki kusikia ushauri wa yeyote ndani ya timu. Wachezaji wa Azam wamekuwa na malalamiko dhidi ya Dabo kwa muda mrefu.

Baada ya kutolewa na Bahir Dar ya Ethiopia kwenye Kombe la Shirikisho la CAF, mchambuzi mmoja wa michezo aliandika kwenye mtandao wake wa instagram matatizo yanayoendelea ndani ya vyumba vya kuvalia vya Azam FC. Mchambuzi huyo ni meneja wa mmoja wa wachezaji wa Azam FC, yawezekana alipewa taarifa na mchezaji wake kwa sababu kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ya klabu hiyo, kila kitu kilikuwa sahihi.

Tofauti ni kwamba wamiliki wa Azam FC wamesema wamechoka kufukuza makocha kila mwaka huku mambo yakishindwa kubadilika. Safari hii wameamua kuziba masikio juu ya malalamiko ya wachezaji na kama itabidi wa kufukuzwa basi wafukuzwe wachezaji lakini siyo kocha. Swali linabaki kuwa, je, wataondoka wachezaji au kocha?

SOMA NA HII  SAMATTA APATA DILI JINGINE, VILLA WAKISHUKA TU ANAIBUKIA HUKU