Home Uncategorized HATMA YA AJIBU KUTUA SIMBA KUJULIKANA LEO

HATMA YA AJIBU KUTUA SIMBA KUJULIKANA LEO

MENEJA wa Ibrahimu Ajibu, Athuman Ajibu amesema kuwa timu atakayojiunga mteja wake itajulikana.

Ajibu alikuwa anatakiwa kujiunga na TP Mazembe dili hilo liliyeyuka kwa kile kilichoelezwa dau kubwa huku akitajwa tayari amemalizana na Simba.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ajibu amesema kuwa kwa sasa mambo bado ni magumu kwake hivyo mpaka jioni atakuwa amemaliza kazi.

“Kwa sasa mambo bado hayajawa sawa, itafahamika leo timu ambayo atajiunga kwani kuna vitu ambavyo ilikuwa bado havijakamilika, kuhusu Mazembe hiyo ishabuma,” amesema Ajibu.

SOMA NA HII  TANZANIA PRISONS YATOSHANA NGUVU NA MTIBWA SUGAR

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here