Home Habari za michezo WENGER KUISAIDIA TANZANIA AFCON ….AANIKA MPANGO MZIMA UTAKAVYOKUWA…

WENGER KUISAIDIA TANZANIA AFCON ….AANIKA MPANGO MZIMA UTAKAVYOKUWA…

Habari za Michezo

Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger amesema atashirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuhakikisha timu ya taifa ‘Taifa Stars’ inakuwa na ushiriki mzuri kwenye fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 ambazo zitafanyika hapa nchini kwa kushirikiana na Kenya na Uganda.

Wenger ambaye ni mkuu wa idara ya maendeleo ya mpira wa miguu ya Shirikisho la soka duniani (FIFA) alisema ili Tanzania iwe na timu imara, inapaswa kufanyia kazi hatua tatu muhimu ambazo ni kutafuta vipaji, kuendeleza vipaji na kuvipa nafasi na idara yake itasaidia katika utimizaji wa mpango huo.

“Kuna vipaji vingi duniani lakini mwishoni havipati vipaji vya kutimiza ndoto zao. Nawaahidi siku moja nitakuja hapa. Kuna kazi kubwa ya kufanya lakini sisi kwa pamoja na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania na FIFA, tutaleta kocha hapa kuelimisha watoto na tutaleta kocha wa kuelimisha makocha.

“Kwa sababu moja kutafuta vipaji, pili kufundisha na kinachofuata ni kukipa nafasi kuonyesha kipaji. Na nyakati katika hatua ya kwanza tunahitaji msaada katika kutafuta kipaji. Tutaleta timu hapa yenye uwezo wa kuorodhesha vipaji na baadaye kwa pamoja na makocha kufundisha vipaji.

“Tuna miaka minne, mitano mbele yetu na kama tutafanya vizuri, nina uhakika tutakuwa na wachezaji wazuri kila eneo,” alisema Wenger.

Wenger alitoa kauli hiyo jana wakati alipotembelea mradi wa ujezi wa kituo cha ufundi cha TFF uliopo Kigamboni, Dar es Salaam ambao uliwekwa jiwe la msingi na Rais wa FIFA, Gianni Infantino na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Patrice Motsepe.

SOMA NA HII  SIKU MOJA BAADA YA AZAM KUMFUKUZA KOCHA WAO MSOMALI...'BWALYA' WA SIMBA AWASHUSHIA LAWAMA WACHEZAJI..