Habari za Simba SC
Habari za michezo

KUHUSU WACHEZAJI SIMBA KUDAI DAI POSHO ZAO….. UONGOZI WAFUNGUKA HAYA

Staff Desk November 18, 2023 11:36 am

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC, Salum Abdallah ‘Try Again’ amesema hakuna mchezi yeyote wa Simba ambaye anadai posho yake.

Try Again ameyasema hayo mara baada ya kuwepo kwa madai kuwa mpasuko ndani ya Simba umesababishwa na baadhi ya wachezaji kutolipwa posho zao.

“Hakuna mchezaji hata mmoja ambaye hajalipwa posho zake, huu ni uzushi ambao hauna maana yoyote. Ni maneno ya wapinzani, ni maneno ya kupuuzwa,” alisema Try Again.

Try Again aliongeza kuwa, Simba ndio timu pekee ambayo inatoa bonus kubwa kwa wachezaji katika mechi na zote zinalipwa kulingana na matakwa waliyojiwekea.

“Mechi ya Al Ahly ya hapa, tuliwaahidi wachezaji wakishinda tutawapa Mil. 500 lakini hawakushinda, mechi ya marudiano tuliwaahidi kuwapa Bilioni moja lakini nayo hawakushinda,” aliongeza Try Again.

AUCHO AFUNGIWA MECHI TATU,REFA COASTAL UNION NA YANGA WAHUSISHWA NJE NUSU MWAKA WAARABU WAPANIA KUVURUGA YANGA……. SASA WATUA KWA MAXI, PACOME

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply