Kufuatia hali ya sintofahamu ndani ya klabu ya Simba, mambo mapya yanazidi kuibuka siku hadi siku haswa kufuatia timu hiyo kutokufanya vyema kwenye baadhi ya michezo.
Ukiachana na kikao cha viongozi ambacho kilikaa jana, ambapo wachezaji walifunguka mambo mengi yanayowasibu, pia kuna jambo ambalo liko nnje ya hayo ambalo soka la Bongo tumefanikiwa kulijua.
Kupitia vyanzo vyetu vya habari, imefahamika kuwa, Simba walikuwa na bajeti ndogo ya usajili ndio maana walisajili wachezaji wa madaraja ya katia ikiwa malengo yao ni makubwa
Miongoni mwa sababu ambazo zimepelekea Simba kusajili wachezaji wa bei ndogo ni boss mkuu kugoma kutoa fedha kwasababu kuna watu ndani ya Simba hawataki Simba ifanikiwe
Hata mkuu wa Scouting wa Simba alileta majina ya wachezaji wazuri kama Yao Kouassi Attohoula, Pacome Zouzouan, Mohamed Zougrane, Milton Karisa, Morrice Chuku,Kagoma pamoja na feisal Salum lakini watu wachache wakafelisha suala la wachezaji hawa kusajiliwa na Simba na watu hao wapo ndani ya Simba
Kocha wa Simba Robertinho alipitisha hawa wachezaji wote na yeye mwenyewe akapendekeza asajiliwe Max Nzegeli kwa kuwa alikuwa anawasiliana nae moja kwa moja lakin baadhi ya viongozi walikwamisha pia mchakato kitu ambacho kilisababisha wakaenda kusajili wachezaji wa kawaida
Chanzo chetu kinaniambia kwamba boss mkuu amegoma kutoa fedha mpaka pale ambapo mambo yatakaa sawa na kuna viongozi ambao anahisi wanamsaliti wakiondoka ataweka tena fedha