Habari za michezo
YANGA WAIPIGA KIJEMBE SIMBA KISA VIKAO VYA USIKU…. KAMWE AFUNGUKA HAYA
Staff Desk
November 30, 2023
12:33 pm
Wakati Yanga wakijiandaa kukabiliana na Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika Klabu ya Al Ahly siku ya Jumamosi Desemba 2 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Ofisa habari wa Klabu hiyo Ally Kamwe amesema ni vyema Mashabiki wakajitokeza kuipa timu hakasa kwa wingi ili kuhakikisha wanamalizana na Ahly hapa hapa nyumbani.
Akizungumza kamwe anasema; “Ukiona mtu anajadili mpira usiku wa manane ujue yamemfika hapa, sasa sisi Yanga SC hatuhitaji kufika huko.
“Sisi Yanga ndio tuna mashabiki bora Afrika na tunaenda kuionyesha Afrika kuwa walikosea kuwapa wale Simba sisi tunaenda kuijaza Benjamin Mkapa, maana vitu vyote wamejifunza kwetu sisi Yanga sasa wanakuwaje bora zaidi yetu.”
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.