Home Habari za michezo AHMED ALLY AWATULIZA MASHABIKI WA SIMBA

AHMED ALLY AWATULIZA MASHABIKI WA SIMBA

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, timu ya Simba SC, imebanwa mbavu nyumbani kwa kulazimishwa sare ya 1-1 na Asec Mimosa ya Ivory Coast.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo kumalizika, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amewatuliza mashabiki wa timu hiyo akisema kuwa kazi bado haijaisha.

“Tumepata alama moja, si nzuri sana na si mbaya sana, Tuna kazi kubwa ya kufanya katika mechi zijazo kuhakikisha malengo yanatimia.

“Bado tuna nafasi ya kufanya vizuri, tumepoteza alama tatu katika 18 za hatua ya makundi hivyo tumebakiwa na 15 za kupigania.

“Nyakati ngumu zinatukomaza na kutukumbusha tuboreshe wapi kwenye timu yetu. Poleni sana Wana Lunyasi.

Msimamo
Galaxy – goli 1, pointi 3, nafasi ya 1
Asec Mimosas – goli 1, pointi 1, nafasi ya 2
Simba Sc – goli 1, pointi 1, nafasi ya 3
Wydad goli 0, pointi 0, nafasi ya 4.

Mechi zijazo
Galaxy vs Simba
Asec vs Wydad

Tangu msimu huu umeanza, Simba haijashinda mchezo wowote wa Kimataifa.

Power Dynamo 2-2 Simba SC
Simba SC 1-1 Power Dynamo
Simba SC 2-2 Al Ahly
Al Ahly 1-1 Simba SC
Simba SC 1-1 Asec Mimosac.

SOMA NA HII  ROBERTINHO ATAMBA KUHUSU KIKOSI CHA SIMBA