Home Habari za michezo HAWA SIMBA, YANGA MBONA KAMA WANATULETEA UTANI KIMATAIFA

HAWA SIMBA, YANGA MBONA KAMA WANATULETEA UTANI KIMATAIFA

Simba na Yanga wote wameanza vibaya katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika kwenye hatua ya makundi baada ya kushindwa kupata ushindi.

Hii ni kama wakeup Call kwao kuelekea michezo ijayo kwenye michezo ijayo kupambana ili kupata matokeo mazuri.

Lakini kuna kitu nakiona sasahivi kwa Simba na Yanga, timu nyingi zinaona kuna mafanikio katika mpira wa Tanzania hivyo zinapocheza na Simba na Yanga zinauma sana meno.

Sio kama miaka iliyopita, timu nyingi zinaamini kuna ubora kwenye ligi yetu,kuna usajili mzuri unafanyika na timu zina pesa kiasi chake.

Sasa kama sisi tutaendelea kucheza kwa mazoea na kuwa tutakwenda Robo fainali basi inaweza kula kwetu msimu huu,mpaka sasa makundi yote ya Simba na Yanga yameonyesha kuwa ni magumu.

Watani mnatakiwa kupambana tunaweza kukosa robo fainali kama tutachukulia poa msimu huu.

SOMA NA HII  ISHU YA NTIBANZOKIZA KUSAINI KCCA UKWELI HUU HAPA