Home Habari za michezo FT: SIMBA 1-1 ASEC MIMOSAS…..PIRA ‘GIMBI MAKANDE’ LAENDELEA MSIMBAZI…

FT: SIMBA 1-1 ASEC MIMOSAS…..PIRA ‘GIMBI MAKANDE’ LAENDELEA MSIMBAZI…

Habari za Simba

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba wameanza hatua ya makundi kwa kusuasua baada kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Hii inakuwa sare ya kwanza kwa Asec Mimosas kupata kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Mara ya kwanza ilikubali kichapo cha mabao 3-1mwaka 2022.

Simba walikuwa kupata bao kwenye mchezo huo lililowekwa kimiani na Saido Ntibazonkiza dakika ya 44 kwa mkwaju wa penalty baada mlinzi wa Asec Mimosas kuunawa mpira ndani ya boksi.

Asec Mimosas walisazisha bao hilo dakika ya 77 mfungaji akiwa ni , N’guessan Pokou, na kuweka mzani sawa kuwa 1-1.

Asec Mimosas walikuwa wa kwanza kulifikia lango la Simba dakika tano kwa mpira wa kona ambao uliokolewa na safu ya ulinzi ya Simba.

Dakika ya saba Asec Mimosas waliendelea kulisakama lango la Simba na kupata kona ya pili ambayo pia iliokolewa safu ya ulinzi ya Simba.

Simba walijibu mapigo dakika ya 13 baada Saido Ntibazonkiza kupiga mpira wa kutengwa uliookolewa na kipa wa Asec Mimosas.

Dakika ya 18 Jean Baleke, alikaribia kuipa uongozi timu yake baada ya kupiga kichwa kilichoenda nje Simba.

Kibu Denis nusura aipatie bao timu yake dakika ya 30 baada ya kupiga kichwa kilichopaa juu ya lango la Asec Mimosas.

Kiungo wa Simba Mzamiru Yasin alikosa bao la wazi dakika ya 39 akiwa ana kwa ana na kipa wa Asec Mimosas Folly Ayayi ambaye aliucheza mpira na kuokoa mpira huo.

Kipindi cha pili kilianza kwa Asec Mimosas kufanya mabadiliko kwa kumtoa Josaphat Bada dakika ya 46 nafasi yake ikachukuliwa na Salifue Diarrassouba ili kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.

Kocha wa Simba Daniel Cadena alifanya mabadiriko dakika ya 59 kwa kuwatoa Jean Baleke na Che Fondoh Malone nafasi zao zikachukuliwa na Moses Phiri na Sadio Kanoute.

Simba walifanya mabadiliko mengine dakika ya 70 kwa kuwatoa Fabrice Ngoma na Kibu Denis nafasi zao zikachukuliwa na Clatous Chama na Luis Miquissone ili kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji.
Simba walifanya mabadiriko mengine dakika ya 86 kwa kumtoa Saido Ntibazonkiza nafasi yake ikachukuliwa na John Bocco.

Kikosi kilichoanza Simba, Ayoub Lakred, Israel Patrick , Mohamed Hussein, Kennedy Wilson, Henock Inonga, Che Fondoh Malone, Mzamiru Yasin, Fabrice Ngoma, Jean Baleke, Saido Ntibazonkiza na Kibu Denis.

Kikosi kilichoanza Asec Mimosas, Folly Ayayi, Beugre Gbakre , Wonlo Coulibaly, Karidioula Mofosse, Josaphat Bada, Anthony Tra bi Tra, Koffi Kouame, Essis Aka, N’guessan Pokou, Frank Zouzoua na Moise Kabore.

SOMA NA HII  BENCHIKHA ATOA KAULI HII KWA MASHABIKI WA SIMBA