Home Uncategorized KOCHA YANGA ATUMIA MIEZI SITA KUISOMA SIMBA

KOCHA YANGA ATUMIA MIEZI SITA KUISOMA SIMBA


 CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa alitumia miezi sita kuwasoma Simba yenye mastaa kibao ikiwa ni pamoja na Luis Miquissone na Meddie Kagere.

Yanga ina kibarua cha kumenyana na Simba, Novemba 7 Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao unasubiriwa na wadau wa mpira ndani na nje ya Bongo.


Kaze amesema kuwa alipokuwa nchini Canada kabla hata ya kusaini Yanga, alipata muda wa zaidi ya miezi sita kuwafuatilia wapinzani wake ambao ni Simba pamoja na timu nyingine ndani ya ligi.

 

“Ukizungumzia ligi ya Tanzania nimeanza kuifuatilia muda mrefu. Miongoni mwa wale ambao nilikuwa ninawafuatilia ni pamoja na Simba, wao najua namna gani wanafanya na mbinu ambazo wanazitumia hivyo sina presha nao pale nitakapokutana nao uwanjani.

 

“Wachezaji wake wengi wapo vizuri hasa ndani ya uwanja na nje ya uwanja pia. Katika hilo, mimi siogopi ndio maana nimekuja kuifundisha Yanga, ninachowaambia mashabiki ni kwamba wasiwe na mashaka katika utendaji wangu,” amesema.


Yanga itawakaribisha Simba ambao ni mabingwa watetezi Novemba 7, Uwanja wa Mkapa mchezo unaoatarajiwa kuchezwa majira ya saa 11:00 jioni.


Msimu uliopita walipokutana uwanjani yalikusanywa jumla ya mabao matano ambapo mchezo wa kwanza, Simba ilitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 kisha ule wa pili Yanga ilishinda kwa bao 1-0, zote zilichezwa Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  MADDISON AGOMEA DILI LA KUIBUKIA MANCHESTER UNITED