Home Habari za michezo BENCHIKHA ATOA KAULI HII KWA MASHABIKI WA SIMBA

BENCHIKHA ATOA KAULI HII KWA MASHABIKI WA SIMBA

Benchikha

Kocha mpya wa Simba SC, Abdelhak Benchikha ametoa kauli nzito na ya kuwapa faraja mashabiki wa klabu hiyo ambao walikuwa wameikatia tamaa timu yao.

Kupitia kwa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema kocha ametoa kauli hiyo iliyobebwa na maneno mawili tu; mafanikio na ushindi.

“Kocha amezungumza winning and success yaani anaahidi ushindi na mafanikio,” alisema Ahmed Ally.

Kocha huyo raia wa Algeria, ameshaanza kazi Msimbazi ambapo kwa taarifa ya awali, leo atakwenda kuona mazoezi na kesho atakuwa na kikao na mazungumzo na mchezaji mmojammoja.

Kama masuala ya vibali yatakwenda vizuri basi kuna uwezekano mkubwa, wikiendi hii akawa mzigoni Simba itakapoenda ugenini kuvaana na Jwaneng Galaxy nchini Botswana Jumamosi Desemba 2,2023.

SOMA NA HII  BENCHIKHA HATAKI MASIHARA AWAACHA MASTAA HAWA KUELEKEA BOTSWANA ISHU NZIMA IKO HIVI