Home Uncategorized NAMUNGO WANACHOKITAFUTA NI HIKI HAPA

NAMUNGO WANACHOKITAFUTA NI HIKI HAPA

KOCHA Mkuu wa Namungo FC, Hitimana Thiery amesema kuwa ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara ni mgumu jambo linalowafanya wawe makini kwenye mechi zao.

Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa kwa sasa mechi zake zilizobaki watapambana kupata matokeo ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea.

“Ligi ina ushindani na kila timu inahitaji ushindi hilo lipo wazi hata sisi pia tunahitaji kupata matokeo mazuri, kwa sasa ni lazima tujipange vema ili kufikia malengo yetu,” amesema.

Namungo ipo nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi zake 51 baada ya kucheza mechi 29.

SOMA NA HII  BERNARD MORRISON NI PASUA KICHWA NDANI YA YANGA, ATIMKA