Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA ASEC MIMOSAS….MASTAA NA MSHABIKI SIMBA WAPEWA UJUMBE HUU MZITO…

KUELEKEA MECHI NA ASEC MIMOSAS….MASTAA NA MSHABIKI SIMBA WAPEWA UJUMBE HUU MZITO…

Habari za Simba

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amewataka mashabiki kusahau yaliyopita na kujitokeza uwanjani.

Ahmed ameyasema hayo leo alipokuwa kwenye mkutano na wanahabari akizindua rasmi kampeni yao ya kuelekea mchezo wao wa kwanza wa hatua ya Makundi Kimataifa dhidi ya ASEC Mimosas.

“Safari hii tunakwenda kuwashangaza watu, tutaujaza uwanja wa Mkapa. Niwambie Wanasimba kama una hasira uje nazo furaha utaikuta uwanjani.”

“Kauli mbiu yetu ya mchezo dhidi ya ASEC Mimosas ni Twendeni Kinyama, Mashabiki Bomba,” alisema Ahmed Ally.

Katika hatua nyingine, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klanbu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa kejeli licha ya kufungwa na watani zao bao 5-1 kisha sare na Namungo FC kwa bao 1-1, bado wana imani na wachezaji wao.

Ahmed amesema hayo leo Novemba 16, 2023 wakati akizindua kampenzi ya hamasa kuelekea mchezo wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa Novemba 25, 2023 katika Dimba la Mkapa.

“Sisi tuko bega kwa bega na wao, lakini tuwakumbushe kwamba yale yote yaliyopita wanapaswa waachane nayo, wasiingie uwanjani wakijihisi wakosefu au wanyonge kwamba tumewapelekea matatizo, waingie uwanjani kifua mbele kuipigania klabu yetu.

“Tuna imani na wachezaji wetu kwamba wanaweza kufanya makubwa na wameshathibitisha hilo, Novemba 25 wakaendeleze hayo makubwa. Tumeteleza hatujaanguka,” amesema Ahmed Ally.

SOMA NA HII  FT: YANGA 5-0 ZALAN FC .....MAYELE ATETEMA KWA HASIRA....AZIZ KI ATOA GUNDU TENA...GEITA GOLD SAWA LAKINI HAITOSHI..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here