Home Uncategorized BOSI AJAX ATHIBITISHA KWAMBA MANCHESTER UNITED WAMEONYESHA NIA KUMTAKA DONNY

BOSI AJAX ATHIBITISHA KWAMBA MANCHESTER UNITED WAMEONYESHA NIA KUMTAKA DONNY


BOSI wa Klabu ya Ajax, Edwin van der Sar amethibitisha kwamba Manchester United imeonyesha nia ya kupata saini ya nyota wao Donny van de Beek.

Nyota huyo aliwahi kukipiga ndani ya United kati ya 2005 na 2011 inaelezwa kuwa United na Real Madrid zinahaha kupata saini yake.

Imeripotiwa na NOS, Van der Sar amesema:”Ipo wazi kabisa kuna timu ambazo zinahitaji saini ya Donny van de Beek ikiwa ni pamoja na Manchester United na Real Madrid.”


 Madrid walikuwa wakitajwa kuitaka saini ya kiungo huyo muda mrefu ila janga la Virusi vya Corona lilitibua mipango ya mazungumzo yao.

Nyota huyo mwenye miaka 23 amekuwa msaada mkubwa ndani ya Ajax jambo lililozivutia timu nyingi.

SOMA NA HII  YANGA WATAJA SABABU ZITAKAZOMPA NAFASI KAZE KUIBUKIA JANGWANI