Home Habari za michezo KUTOKA TANZANIA,BURUNDI MPAKA BAYERN MUNICH

KUTOKA TANZANIA,BURUNDI MPAKA BAYERN MUNICH

Shirikisho la Soka la Burundi bado linatumai kumshawishi Nestory Irankunda kuchezea nchi ya wazazi wake baada ya kijana huyo kukubali kuhamia kwa wababe wa Ujerumani Bayern Munich.

Fowadi huyo wa Adelaide United mwenye umri wa miaka 17 alizaliwa katika kambi ya wakimbizi nchini Tanzania na sasa anaishi Australia, na ameiwakilisha nchi hiyo katika ngazi ya chini ya miaka 17.

Tayari amekuwa sehemu ya kikosi cha Australia, baada ya kuwa mbadala wa Socceroos wakati wa mechi mbili za kirafiki dhidi ya Ecuador mwezi Machi.

“Tungependa achezee Burundi lakini ana ndiye mwenye uamuzi wa mwisho – anaweza au asije kucheza kwa niaba yetu,” rais wa FA wa Burundi Alexandre Muyenge aliambia BBC Sport Africa.

SOMA NA HII  JKT TANZANIA NA SOKO LA USAJILI DIRISHA DOGO