Home Habari za michezo MAN CITY, CHELSEA MAMBO SIO MAMBO TENA

MAN CITY, CHELSEA MAMBO SIO MAMBO TENA

Baada ya Everton kupokonywa alama 10, taarifa zinadai kwamba mabosi wa timu za Manchester City na Chelsea wako matumbo ni joto wakihofia kunyang’anywa alama zitakazozishusha kwenye nafasi za sasa.

Everton imepokonywa alama hizo baada ya kukutwa na hatia ya kukiuka sheria ya usawa wa matumizi ya pesa na sasa ipo kwenye hali mbaya zaidi baada ya Leeds, Leicester City, Southampton, Nottingham Forest na Burnley kuidai fidia.

Wataalamu wa masuala ya kisheria wameionya Man City, ambayo Januari, mwaka huu ilituhumiwa kwa makosa 115 ya kukiuka sheria hiyo sambamba na Chelsea ambayo ipo chini ya uchunguzi ikidaiwa kukiuka sheria hiyo enzi za umiliki wa Roman Abramovic.

Kwa mujibu wa mmoja kati ya wanasheria mahiri wa masuala ya michezo nchini England, Stefan Borson ambaye pia aliwahi kuwa mshauri wa masuala ya kifedha wa Manchester City ni kwamba, kama Man City au Chelsea zitakutwa na hatia, basi zinaweza kushushwa daraja.

Borson alidai adhabu iliyopewa Everton ni ndogo kwa kosa ililofanya na mambo yanaweza kubadilika kwa Man City na Chelsea ambazo huenda zikakumbana na adhabu kali ya kuzishusha daraja.

Hata hivyo, Man City ilikana tuhuma za kukiuka sheria na ikaajiri mwanasheria NGULI kutoka kampuni ya KC Lord Pannick kwa ajili ya kuitetea kwenye kesi hiyo.

Everton ilikutwa na hatia ya kuzidisha matumizi ya Pauni 19.5 milioni kutoka Pauni 105 milioni ilizotakiwa kutumia ikifanya hivyo kwa miaka mitatu. Lakini, kwa upande wa Chelsea na Man City inaonekana kwamba zitapata adhabu kubwa zaidi kwa sababu zimekuwa zikihusishwa kukiuka sheria kwa muda mrefu, hivyo hata adhabu itakuwa kubwa tofauti na Everton.

SOMA NA HII  GAMONDI ALIAMSHA AKATAA UTARATIBU HUU WA VIONGOZI WA YANGA