Home Habari za michezo MANARA AKABIDHIWA KIPAZA SIKU YA MCHEZO WA MOROCCO

MANARA AKABIDHIWA KIPAZA SIKU YA MCHEZO WA MOROCCO

HAJI MANARA AUMBUKA...NI BAADA YA KUMGOMBANISHA RAISI YANGA NA MTANGAZAJI

Kila mmoja wetu Mungu amemtunuku kitu special vile atakavyo. Wengi tuko tofauti katika vitu vingi, japo muda mwingine tunaweza kufanana katika hili na lile.

Jumanne tuna mechi ngumu kama nchi. Ni ngumu mno. Hii ni ngumu zaidi ya neno ngumu lenyewe. Kama Taifa tulipaswa kuitumia kila aina ya silaha tuliyonayo kumpiga adui Morocco.

Hapa ndiko anakoingia Haji Sunday Ramadhan Manara. Kinywa chake kinahitajika katika mechi hii. Haji ni moja ya silaha tulitonayo katika ghafla letu.

Haji ana ulimi wa kuujaza uwanja. Amewahi kufanya hivyo mara nyingi tu. Siandiki / sisemi haya kwa kuwa niko Manara TV na nimeamua kumsifia Boss wangu. Hapana! Jamaa anastahili.

Maana tunajuana. Baada ya mtu kuanza kuishambulia hoja iliyoko mezani mwake anaweza kuanza kumshamvulia mtoa hoja ambaye hamuoni na hayuko mezani mwake. TUNAJUANA.

Mechi ya Jumanne inakihitaji kinywa cha Haji kuhamasisha watu kuja kuujaza uwanja. Ushindi wa jana pale Morocco umerahisisha vitu vingi vya kuufanya uwanja ujae.

Mashabiki wetu wamezoea kuambiwa maneno fulani fulani hivi. Iandaliwe Press. Hapa Bongo Zozo na Manara, pale Hersi, Rais Karia na Try Again. Kisha yapigwe maneno na ikiwezekana kiingilio kiwe bure. Ikiwezekana lakini. Mechi hii tunataka alama tatu, hatutaki pesa.

Mechi za namna hii lazima tutumie watu tulionao kwenye masuala ya ushawishi katika mpira wetu ili kupata Full House pale kwa Mkapa.

Tanzania ni wamoja.

Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Taifa Stars.

SOMA NA HII  MJUMBE WA BODI AFICHUA DATA ZA SIMBA KWA WAARABU....UKWELI NA ISHU NZIMA IKO HIVI...