Home Habari za michezo SIKU YA KWANZA TU KAZINI…BENCHIKHA AWAPIGIA MAGOTI MASHABIKI SIMBA….KILIO CHAKE HIKI HAPA…

SIKU YA KWANZA TU KAZINI…BENCHIKHA AWAPIGIA MAGOTI MASHABIKI SIMBA….KILIO CHAKE HIKI HAPA…

Simba SC

Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Abdelhak Benchikha amesema kuwa hataangalia jina la mchezaji bali atapanga mchezaji kulingana na performance yake kwenye uwanja wa mazoezi.

Benchikha amese hayo jana Jumanne, Novemba 28, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa kumtambulisha rasmi kuanza kuitumikia klabu hiyo.

“Nina furaha kubwa kuwepo hapa. Tangu nilipoanza kuwasiliana na viongozi nilikuwa na shauku ya kuja. Jambo kubwa ambalo naomba ni mashabiki kutupa ushirikiano na naamini kupitia hilo tutafanikiwa pamoja.

“Kuna mambo mengi ambayo tayari nayajua na nimekuja na mikakati ambayo nitaifanyia kazi. Kuhusu wachezaji nitajua zaidi nikishaanza kazi, kuhusu mashindano ya ndani na kimataifa yote ni muhimu. Mimi ni mpambanaji na nitapambana hadi tutafika.

“Mafanikio yatajengwa na Wanasimba wote hilo ndio muhimu zaidi. Kwa wachezaji sitaangalia majina bali anayefanya vizuri, kiwango cha mchezaji ndio kitafanya nimtumie,” amesema Benchikha.

Benchikha amesajiliwa na Simba baada ya kuachana na USM ALger akiwa ameshinda Ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika kwa kumtoa Yanga pamoja na ubingwa wa Super league kwa kumfunga Al Ahly.

SOMA NA HII  UKWELI WA STORI ZA 'JEANS' LA MGUNDA NA MAMBO YA KIFREEMASON...