Home Habari za michezo TRY AGAIN:- KWA SIMBA HII BADO SANA …SISI DOLA MIL 1 ...

TRY AGAIN:- KWA SIMBA HII BADO SANA …SISI DOLA MIL 1 NI USAJILI KWA TIMU NZIMA…

Habari za Simba SC

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Salum Abdallah ‘Try Again’ amesema kama klabu na Taifa la Tanzania, bado kuna safari ndefu ya kufikia mafanikio katika soka.

Try Again ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano maalum na Azam TV akielezea masuala mbalimbali ikiwemo zawadi ya mashabiki bora waliyoipata kwenye mashindano ya African Football League (AFL).

“Tau (Percy) analipwa dola laki nane kwa mwaka, aliyekuwa anacheza naye Tshabalala labda ni ten parcent ya hiyo kwa mshahara wake kwa mwaka, unaweza kuona tofauti ya madaraja. Kipa yule wa Al Ahly analipwa takriban dola elfu hamsini, sitini na kuendelea.

“Kipa wetu aliocheza nafikiri mshahara wake na signing fees zake zote haziwezi kuzidi dola elfu mbili au elfu tatu kwa mwezi. Tuanayo safari ndefu ya kufikia mafanikio hatua kwa hatua,” alisema Try Again.

“Mamelodi wana wachezaji Chile, Brazil dola Miloni tatu, Milioni mbili sisi dola Milioni moja ni usajili wa timu nzima kwa mwaka, kwa hiyo huwzei kwenda mbinguni kabla hujafa, lazima tukubali kwamba tunahitaji kufanya kazi, tunahitaji kuwekeza zaidi,” alisema.

SOMA NA HII  SHINDA KWA KUCHAGUA NAMBA ZAKO TANO ZA BAHATI NDANI YA SLOT YA CIRCUS FEVER...