Home Habari za michezo UNAMBIWA HUYO MUSONDA HUKO YANGA NI KUWA KAZINI KWAKE KUNA KAZI

UNAMBIWA HUYO MUSONDA HUKO YANGA NI KUWA KAZINI KWAKE KUNA KAZI

Habari za Yanga

Straika wa Yanga, Kennedy Musonda katika dakika 411 alizocheza kwenye mechi saba, kafunga mabao mawili dhidi ya JKT Tanzania na Simba akifunikwa na mawinga Aziz Ki na Maxi Nzengeli ambao ni vinara wa mabao.

Kwenye mechi tisa za Yanga, ikishinda nane na sare moja, ikiongoza kwa pointi 24 na mabao 26, Musonda alicheza dhidi ya KMC (dakika 64), JKT Tanzania (78), Namungo (90), Geita Gold (17), Singida Big Stars (18), Simba (72) na Coastal (72).

Hadi sasa Ki na Nzengeli wamefunga mabao saba na asisti mbili kila mmoja, hivyo wamechangia zaidi ya nusu ya mabao 26 ya Yanga, jambo ambalo wataalamu wa soka wameliona kama ni alamu kwa Musonda kuonyesha heshima ya nafasi yake, kwani walimtarajia kufunga sana baada ya kuondoka Fiston Mayele.

Ili kuthibitisha Musonda anapaswa kukaza buti, kauli ya kocha wa timu hiyo, Miguel Gamondi kuwa anahitaji kiungo na straika inapaswa kumuamsha zaidi.

Straika wa zamani wa timu hiyo, Said Bahanuzi alisema kocha anapoongeza nguvu kuna mambo mawili, β€œushindani zaidi wa kila nafasi au wapo hawajampa matokeo ya kile anachotaka. Yanga wanafunga mawinga sababu wapo kwenye upepo huo. Kuna wakati wanaweza wakakwama.”

Beki wa zamani wa timu hiyo, William Mtendamema alisema laiti kila mchezaji akiwajibika ipasavyo kwenye nafasi yake hakuna kocha anayeweza kuumiza kichwa namna ya kupanga kikosi.

SOMA NA HII  UCHOCHORO WA SIMBA KUWA KIBONDE UKO HAPA