Home Habari za michezo UNAAMBIWA YANGA WAMESHASAHAU MATOKEO YA ALGERIA

UNAAMBIWA YANGA WAMESHASAHAU MATOKEO YA ALGERIA

Habari za Yanga leo

Nahodha wa Yanga, Bakar Mwamnyeto amesema wamesahau matokeo ya Algeria na leo ni kazi moja tu kuhakikisha timu hiyo inapata ushindi.

“Sisi kama wachezaji tumejipanga vizuri tayari kwa ajili ya kuhakikisha tunaopata ushindi nyumbani, hiyo ni lazima. Tumejipanga na makosa yote ya mechi ya kwanza tumeyafanyia kazi na Inshallah kwa jinsi tulivyojipanga ni kuona tunashinda,” alisema Mwamnyeto ambaye hakucheza mchezo wa kwanza wa Algeria baada ya kocha Miguel Gamondi kuwatumia Dickson Job na Ibrahim Bacca.

Nahodha huyo aliyekuwa kwenye kikosi cha Yanga kilichotwaa mataji saba tofauti ndani ya misimu miwili ya Ligi Kuu Bara, Kombe la ASFC na Ngao ya Jamii na Kombe la Mapinduzi 2022, huku akicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger na kulikosa taji kiduchu kwa kanuni ya faida ya bao la ugenini baada ya mechi zote mbili kumalizika kwa sare ya 2-2, alisema kila mcheza ana mzuka wa ushindi.

“Hii ni mechi ngumu, lakini tumeshafanyia kazi makosa na tunaenda kuikabili Al Alhy tukiwa tumejipanga kwelikweli ili tuvune pointi tatu kundini.”

Yanga ikiibuka ushindi kwenye mchezo wa leo utakuwa ni pointi tatu za kwanza kwao kwenye michuano hiyo tangu 1998, kwani iliposhiriki makundi ya Ligi ya Mabingwa, iliishia kuambulia sare mbili tu.

SOMA NA HII  YANGA : AL MAREIKH WANAKUFA NYINGI